| |
    


|
2.1.0 SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
2.1.1
Shabaha
Kufikia mwisho wa mafunzo ya kiswahili katika shule ya upili
mwanafunzi aweze:
- kubainisha maana na dhima ya lugha;
- kueleza misingi ya uainishaji wa
maneno ya Kiswahili;
- kukuza uwezo wa kutumia sauti, maneno
ya Kiswahili sanifu katika mawasiliano ya kimazungumzo na kimaandishi;
- kutambua na kurekebisha makosa ya
kisarufi na matumizi ya lugha/kimantiki;
- kukuza uwezo wa kutumia msamiati na
istilahi;
- Kufafanua maana na aina za tungo;
- Kuchanganua sentensi na kufafanua
maana, aina na vijenzi vya sentensi.
2.1.2 Yaliyomo
1.
Lugha
a) Maana na dhima ya lugha
b) Sauti: Irabu/vokali, Konsonanti,
Mpangilio wa sauti katika silabi na maneno
c) Vipashio vya lugha: sauti-silabi-neno-
sentensi
2. Misingi ya maneno
a) Mofimu:
i) Maana na
ii) Aina
- Huru
- Tegemezi
b) Viambishi –
i) maana na
ii) aina
- Awali
- Tamati
3. Aina za maneno na migawanyiko yake:
Aina
za maneno
a) Nomino N - jumla/kawaida, pekee,
dhania, kitenzi jina, jamii, na nomino za wingi.
b) Vivumishi V – sifa, , vionyeshi,
vimilikishi, viulizi, idadi, pekee, majina, unganifu,
virejeshi, na visisitizi
c) Vitenzi T - vitenzi halisi, vitenzi
vikuu, visaidizi, vishirikishi vipungufu, vishirikishi vikamilifu, na
vitenzi
sambamba
d) Viwakilishi N – vionyeshi,
vimilikishi, viulizi, virejeshi, ‘A’ unganifu, sifa, nafsi, ngeli,
pekee, idadi,
visisitizi, na ‘O’ rejeshi
e) Vielezi E - Vielezi vya:
i) Namna/jinsi – vikariri, halisi,
mfanano, hali, ala/vitumizi, na viigizi.
ii) Wakati – viambishi na idadi/jumla
iii) Idadi/Kiasi - idadi halisi na
maneno kamili
iv) Mahali – viambishi na maneno
kamili
f) Viunganishi U
g) Vihusishi H
h) Vihisishi
Ukurasa wa
1
2
3
4 5 6
7 8
Chumba cha Majadiliano>>>
Tuma Maswali/majibu>>> |
|