|
Chumba cha Majadiliano>>>
Tuma Maswali/majibu>>>
UTANGULIZI
Kufuatana na mfumo wa
silabasi mpya uliowekwa na Taasisi ya Elimu ya Kenya ili kuimarisha na
kuendeleza lugha ya Kiswahili baina ya wasomaji na wazungumzaji,
kulipitishwa kuwa kipengele cha isimu –jamii kirudishwe tena katika somo
la Kiswahili. Hiki ni kipengele ambacho zama za zama kilikuwa
kinafundishwa shuleni na hata vyuoni lakini kwa sababu moja au nyingine,
kikawekwa kando. Kurudishwa tena kwa kipengele hiki cha lugha katika
silabasi mpya ni jambo murua na la kujivunia sana hasa tunapozingatia
kuwa mwacha mila ni mtumwa na pia kuwa hii ni njia mojawapo ya
kuonyesha na kudhihirisha kukua kwa lugha kutoka kizazi kimoja
hadi kingine.
Hata hivyo, jambo hili
limewawia kizungumkuti mahuluki lukuki madhali isimu jamii ilikuwa
imetupiliwa mbali katika kaburi la sahau. Iliyokufa fo! Habari njema ni
kuwa, hakuna refu lilsilokuwa na ncha kwani uozo huo umefikia
kikomo.Itakuwa ni dhambi kama si kosa au hatia nisiposhughulikia baadhi
ya istilahi au msamiati unaotumiwa katika lugha ili kuiondoa siutafahamu
iliyoko kuhusu maneno anuwai na pia ili kukuangazia wewe msomaji upevuke
juu ya yale unayoyasoma.
Isimu (linguistics)—ni
mtalaa ambao huchunguza, huchanganua na pia kuchambua na kufafanua lugha
kama
mfumo wa mawasiliano baina ya wanadamu.
Isimu-Jamii—ni
mtalaa unaochunguza lugha ikiwa katika muktadha wake wa matumizi na
wanaoitumia –jamii.
Lugha
-- ni mfumo wa mawasiliano
unaotumia mpangilio maalum wa sauti kuunda vipashio vikubwa zaidi k.m.
mofimu, neno, sentensi n.k. Ni mfumo wa sauti ishara na masolugha.
Lahaja—haya
ni matumizi tofauti ya lugha moja kulingana na mazingira ya mzungumzaji.
Lafudhi—haya
ni matamshi au namna ya kutamka maneno katika lugha fulani.
Lugha ya Taifa—lugha
inayotumiwa kuwatambulisha na kuwaunganisha wananchi wa nchi au jamhuri
fulani ili
kuweza kutambulika na pia kuendeleza muiano na utangamano.
Lugha sanifu—hii
ni lugha ambayo imefanyiwa marekebisho na ukarabati anuwai ambapo
wanaoisanifisha
huafikiana kuhusu vipengele mbalimbali.k.m. Fonimu,
Mofolojia, Sintakisia, semantiki na msamiati.
Lugha rasmi—ni
lugha inayoteuliwa katika nchi fulani ili kutumiwa katika mawasiliano
yaliyo rasmi katika nchi
husika k.m. Kiingereza.
Lugha rasimi—huwa
ni mtindo fulani wa lugha hasa uliotumiwa zamani na watu mashuhuri na
ukaaminika kuwa
kuwa ni mtindo bora wa lugha unaofaa kuigwa na wengine.
K.m. ule uliotumiwa
na William Shakespeare,
Kigiriki, n.k.
Lugha mame—hii
ni lugha ambayo bado haijakua na imo katika umbo lake la awali.
Lugha azali—hii ni lugha
ambayo huzaa lugha zingine au nyingine.
Misimu—ni
lugha ya kisiri ambayo hutumiwa na kikundi fulani cha watu katika jamii
k.v. kwa kutumia mafumbo au
lugha –simo (Sheng’)
Pijini—hubuniwa
kwa kukopa msamiati kutoka lugha mbalimbali ili kutumika kwa mawasiliano
baina ya watu
ambao lugha zao ni tofauti na hawana lugha moja
wanayoielewa.
Krioli—ni
lugha ambayo hutokana na pijini kukua, kukomaa , kupevuka na kuendelea.
Baadhi ya sajili za lugha
ni kama vile: Lugha ya Mahakamani, Dini, Sokoni, Magazetini,
Mahojiano, Simu, Wanahirimu, Wataalamu, Majambazi, Hospitalini,
Mapenzi, Michezoni, Utambaji, Matatu, ya Taifa, Biashara, Mazishi-Matanga,
Kawaida, Wanasiasa, Ofisini, Wazee, n.k..
Kwa makala zaidi kuhusu
sifa na mifano ya sajili au rejista mbalimbali za lugha, jinunulie
nakala yako ya kitabu cha ‘Nuru ya Isimu Jamii-Na David W. Ndegwa’,aliye Mlezi wa Jopo la Kiswahili la Shule ya Upili ya Starehe na pia mwalimu aliyebobea katika Lugha Tukufu ya Kiswahili shuleni
mumo humo.
|